Bunge la Kitaifa limempiga marufuku Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki EALA Falhada Iman dhdii ya kuingia katika majengo ya Bunge katika kipindi cha siku 90 baada ya kunaswa katika video akizabana makofi na Mbunge Maalum Umulkher Mohamed, Jumanne Aprili, 8.

Sheria ya Tume ya Huduma za Bunge inawaruhusu waliokuwa wabunge na Wabunge wa EALA kuingia katika majengo hayo ya bunge na maeneo mengine katika mabunge hayo sawa na wenzao wanaohudumu.

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, amemwagiza Falhada kuwasilisha barua rasmi ya kuomba msamaha kwa Bunge na Kamati ya Huduma za Bunge PSC ifikiapo tarehe 14 Aprili saa kumi na moja jioni.

“The Honourable Falhada is precluded from accessing the precincts of Parliament for a period of 90 days, except for the day she will deliver her apology to the Speaker, on which she will be escorted by the Sergeant-at-Arms,” Wetang’ula alisema.

Kulingana na Spika, baada ya kuikagua video iliyosambazwaa mitandaoni iliyowaonesha wawili hao wakizabana makofi aliamua kuwapa nafasi ya kujieleza.

Alisema,  “Several members, aggrieved by the incident, have approached me and asked that I invoke Parliamentary Powers and Privileges under Cap 36 and refer the matter to the Powers and Privileges Committee,”

Wetang’ula aliongeza kuwa atatoa mwelekeo zaidi baada ya Mbunge huyo wa EALA kuwasilisha rasmi hoja ya kujieleza na Mbunge Umulkher kuomba bunge msamaha.

 Spika alisema hivi “Having reviewed the video and the incident report, it is evident that both Honourable Falhada and Honourable Harun cast Parliament in a bad light and reflected adversely on its integrity, dignity, and the sanctity of the institution,”

Makabiliano baina ya wabunge hao wawili  yameibua maswali mengi nchini huku Wakenya wakiwashtumu vikali wakisema wanastahili kuwa vielelezo katika jamii.

Tayari Mbunge huyo wa EALA ameomba umma msamaha kufuatia tukio hilo la Jumanne.