Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amejitokeza kukashifu vikali serekali kufuatia kufyatuliwa kwa vitoza machozi kwa wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Butere.
Kalonzo ametaja kama aibu kubwa kwa taifa kwa jambo kama hilo kutokea akipongeza wanafunzi hao kwa ujasiri wao.
Ameandika hivi katika mtandao wake wa X (awali Twitter),“What a national shame! How does this regime justify lobbing teargas at young girls from Butere Girls who declined to stage their play “Echoes of War” at the National Drama Festival? Their bravery serves as a national wake-up call. When voices of truth are silenced and art is censored, democracy suffers. I stand with Butere Girls and all students who joined the walkout in solidarity. Kenya must remain a country where even the echoes of war are heard — and heeded. The silence from State House, the Ministry of Education and the Ministry of Interior is absolutely telling”
Pia, Kalonzo ametaja kukamatwa kwa Malala kama kukiuka Katiba inayompa kila mkenya uhuru wa kujieleza
Ikumbukwe kuwa mchezo wa kuigiza wa Echoes of war ilizua gumzo mtandaoni na mitaani baada ya kupigwa marufuku japo Mahakama ya juu mjini Nyamira ilitoa uamuzi ulioruhusu uigizwe katika tamasha za kitaifa katika Shule ya Melvin Jones Academy.
Hivi sasa, Malala aliyekamatwa Jumatano usiku ameachiliwa huru huku wanafunzi wa Butere wakiandikisha historia baada ya kuingia ukumbini na kuimba wimbo wa taifa kisha kuondoka bila kuigiza kama ilivyoratibiwa.