Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu ya Kenya (KeNHA) imetangaza kutatiza kwa siku nne trafiki katika sehemu ya barabara kuu ya Thika na masaa machache kwa sehemu za malipo(toll stations) za Mlolongo na lango la barabara ya moja kwa moja (Expressway) Syokimau.

Katika notisi kwa umma, mamlaka hiyo imekiri kufungwa kwa muda kutaathiri sehemu ya barabara kuu ya Thika Superhighway(S1) iliyoko Kihunguro.

Sehemu iliyoathiriwa itafungwa kuanzia Ijumaa, Aprili 11, 2025 hadi Jumatatu, Aprili 14, 2025, kati ya 11:00 jioni na 4:00 asubuhi.

“The Kenya National Highways Authority (KeNHA) would like to inform the public of a temporary traffic disruption following the closure of a section of Thika Superhighway (S1) Road at Kihunguro, from Friday, April 11, 2025, to Monday, April 14, 2025, between 2300 hrs and 0400 hrs. This is to allow for highway maintenance works along the section,” KeNHA imetangaza

Madereva wanaosafiri kutoka Nairobi hadi Thika, pamoja na wale wa Thika kuelekea Nairobi,wanashauriwa kutumia njia za huduma (service lanes) kama ilivyoonyeshwa kwenye mpango wa usimamizi wa trafiki.

Watumiaji wote wa barabara wanatakiwa kuzingatia hatua za usimamizi wa trafiki, ikiwa ni pamoja na kufuata alama za barabarani, na kushirikiana na polisi na wakuu wa trafiki ili kuhakikisha mtiririko mzuri wa trafiki na usalama wakati wa matengenezo.

“Motorists travelling from Nairobi to Thika and vice versa are advised to use the service lanes as indicated in the drawing or as directed by traffic marshals,”KeNHA imeshauri.

Vile vile, Kituo cha malipo cha Mlolongo na lango la Syokimau A(Mkabala na Dinlas Pharma) zitasalia kufungwa Jumamosi tarehe 12 Aprili,2025 kuanzia saa nne jioni hadi Jumapili tarehe 13 Aprili,2025 saa mbili asubuhi ili kuwezesha ujenzi unaoendelea.

“Please note that Mlolongo Toll Station and Syokimau entrance A(Opposite Dinlas Pharma) will remain closed on Saturday 12th April, 2025 from 10:00pm to Sunday 13th April, 2025 at 8:00am to pave way for ongoing construction of the pedestrian overpass at Katani area. CBD bound motorists using the Mlolongo and Syokimau entrances are advised to use the SGR entrance while Mlolongo bound motorists are advised to use JKIA exit. Please plan your trips accordingly as closure will significantly affect traffic. Apologies for the inconvenience caused,”yasoma tangazo la KeNHA.