Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya amekamatwa mjini Nairobi kufuatia operesheni kali iliyofanywa na maafisa wa polisi.

Mshukiwa kwa jina George Odhiambo Owuor amekamatwa akisafirisha akiwa na kilo   hamsini ya bangi na misokoto elfu moja mia tatu hamsini ya bangi.

Pakiti mia nne za dawa za kuelvya aina ya Razzle, sigara elfu sita  na mashine mbili za kupimia uzani pia vimepatikana.

Mshukiwa anayeaminika kuwa mhusika mkuu wa usafirishaji wa dawa za kulevya anaendelea kuhojiwa akisubiri kufikishwa mahakamani.