Taharuki imetanda katika kijiji cha Kegoye kwenye kata ya Lugaga, Vihiga baada ya mabaki ya mwili wa binadamu kupatikana katika shamba moja lililo karibu na mto kijijini humo.

Haijabainika mwathiriwa huyo ni nani huku polisi wakianza uchunguzi kubaini kiini cha kifo chake.

Mabaki ya mwili huo yaligunduliwa na mvulana aliyekua ameenda kutema kuni Ijumaa mchana. Kulingana na mvulana huyo, fuvu la kichwa lilikua kando na mwili huku wanakijiji waliofika kwenye eneo la tukio wakieleza kuwa huenda mwili huo umekua katika sehemu hiyo kwa muda mrefu

Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI kwa ushirikiano na polisi wa kawaida waliuondoa mwili huo. Wakazi wa Kegoye wameeleza kushangazwa na tukio hilo huku wakitaka uchunguzi wa haraka kufanywa ili kumtambua mwendazake na pia kiini cha kifo chake

Kisa hiki kinajiri wiki mbili tu baada ya mwili wa mtu mwingine kupatikana katika shamba la mahindi kwenye eneo jirani la Mukingi. Wakazi wanataka usalama kuimarishwa.

Written by Arnold Adidi