Maafisa wa Idara ya Upelelezi wanamzuilia mwanaume mmoja anayedaiwa kutekeleza ulaghai mjini Mombasa.
Kwa mujibu wa DCI, mwanamume huyo alikodisha ‘Airbnb’ yenye vyumba vitatu kwa muda wa wiki mbili, yenye thamani ya Shilingi 370,300, kisha akatoweka bila kulipa bili hiyo hilo.
DCI ilieleza kuwa mshukiwa pamoja na wenzake wawili walianza mpango huo kwa kutuma ujumbe wa malipo wa RTGS kwa KSh105,800.
Hata hivyo, fedha hizo hazikuonekana katika akaunti ya mwenye nyumba.
Wakati mwenye nyumba alipofuatilia malipo hayo, mshukiwa alimhakikishia kwamba kampuni yake ingetatua bili yote kabla ya kuondoka.
Taarifa ya DCI ilisema, “They first sent an RTGS message for Sh105,800, but the funds never reflected in Airbnb’s account. When the host inquired about the missing payment, the suspect confidently claimed that his company would cover the bill before their departure.”
Hata hivyo, watatu hao walitoroka bila kulipa deni hilo.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa mshukiwa huyo ana historia ya kuwalaghai watu wasiofahamu katika nchi mbalimbali barani Afrika.
Maafisa wa upelelezi pia wamemhusisha na kisa kingine cha awali ambapo yeye na wenzake waliripotiwa kuilaghai hoteli nyingine jijini Mombasa kwa kutumia mbinu kama hiyo.
Mshukiwa anaendelea kuziliwa akisubiri kufikishwa mahakamani huku maafisa wa usalama wakiwasaka washirika wake.
Nchini Kenya, ujumbe wa malipo wa RTGS hushughulikiwa kupitia Mfumo wa Malipo wa Kielektroniki wa Benki Kuu (KEPSS), unaosimamiwa na Benki Kuu ya Kenya. KEPSS huruhusu uhamishaji wa fedha wa papo kwa papo kati ya benki kwa malipo yenye thamani kubwa au yanayohitaji haraka.