Hali ya Taharuki inazidi kutanda kwenye Eneo Bunge la Mlima Elgon Kaunti ya Bungoma kufuatia utata wa Mti wa aina ya Mkuyu unaominika kuwa na miaka laki tatu .
Makundi mawili yakemuwa yakizozania mti huo ,kundi moja likitaka ung’olewe baada ya Tambiko kwa madai ya kuimarisha amani na maendeleo eneo hilo
Katika kijiji cha Toroso, Eneo bunge la Mlima Elgon mti huo ambao unaaminika kuwapo kwa miaka na mikaka, umezua utata .
Jumatano asubuhi kulishuhudiwa vuta n’kuvute baina ya uongozi wa Eneo Bunge hilo na kundi la wazee linalotaka kung’oa mti huo.
Maafisa wa Polisi wakishika doria kutuliza hali.
Kulingana na Chemaket Edwin, mmoja wa viongozi wa wazee hao anasema kuwa walipania kuwa na mkutano na Kamishna wa kaunti ya Bungoma kuhusu tambiko la kabla ya kung’oa mti huo.

“Sisi (Coordinator)kama wazee tumekuwa tukifanya maneno ya patanisho mlimani tangu mwaka 2017 mpaka 2021 ambako tulikomeshwa kwa sababu ya kisiasa,Na kurejelea tena shughuli yetu ya kufanya matambiko ili kusafisha mlima ili kuleta amani bado inakumbwa na Pingamizi. “
Chemaket anasema kuwa mkutano huo uliokuwa ufanyike ukiongozwa na Kamishna wa Kaunti ya Bungoma Thomas Sankei ulitibuliwa na kundi linaloongozwa na Mbunge wa eneo hilo Fred Kapondi kwa kauli kuwa mkutano ulikuwa umehairishwa Mwanzoni.
“Juzi Kamishna Sankei alikuwa ameitisha Mkutano ili kujadili na wenyeji kutathmini hatari ya Mti (Mkuyu) ambao umekoma sana,utang’olewa aje,Lakini kufikia saa moja na nusu tunaambiwa mkutano hakuna, tuliweza kuwaarifu wenzetu wa Transnzoia tukawazuia wale Kapsokwony, wenye hawakupata habari bado walikuja mpaka Toroso na kukuta Maafisa wa Polisi wamepigw Doria, baadaye mbunge alifika na watu wake na kuvamia wazee ,wengine wakijeruhiwa,Askari wakijionea tu Filamu.”
Kauli hiyo imetiliwa mkazo na mzee Joseph Jepkirui ambaye ni kiongozi wa Jamii ya Sabaot, Kaunti ya Bungoma na Ile ya Trans-Nzoia akikashfu uvamizi uliotekelezwa na Mbunge Fred Kapondi hata na mwandishi wa Babari aliyekuwa anafuatilia taarifa hiyo ya Mkuyu.
“Ile kitu tunakemea sana ni kunyanyaswa , tunashikwa ,familia zinapigwa bila sababu ,Suala ambalo lilifanywa miaka mingi iliyopita.Tumeamua kutoka Cheptais Mpaka Swam tutakuwa tukidumisha Tamaduni zetu ili tuendelee kuishi Kwa Amani.
Wamemtaka Mbunge Fred Kapondi kuwa kipaumbele katika juhudi za amani katika eneo hilo na kuwalinda wananchi kwa jumla huku wakisistiza kuwa lazima watang’oa Mkuyu huo ambao unaaminika kuwapo kwa takribani miaka mia tatu.
Lakini je, mbona makundi hayo mawili yanazozania ,mti huo ? Ni swali ambalo kila msomaji angetaka kujua siri ya Mkuyu wa Toroso.
Kulingana na Chemaket ni kuwa chini ya kisina cha Mkuyu huo kuna Kengele, inayoashiria kufuga ng’ombe na baada ya kufungiwa, ufugaji umedorora, akisema kuwa pia kuna jembe liitalwo (Kosiriondeti) jembe la Kisabaaot linaominika kutumika kupalilia Wimbi.
“Hivyo vifaa viwili kama havitatolewa, mlima utendelea kuwa masikini na chakula kitaendelea Kupungua,hata wewe unaona mwaka huu mpaka lori zinaleta chakula cha msaada Mlimani”Chemaket alisistiza
Mbunge wa eneo hilo Fred Kapondi amekuwa akipinga kundi hilo ambalo limebuniwa kuwa kikundi cha fimbo ambacho anahofu kitasababisha kudorora kwa amani katika eneo hilo.
Katika mkutano wa usalama uliofanyika wiki chache zilizopita katika kijiji cha Kopsiro ukiongozwa na Kamishna Thomas Sankei, Kapondi alisema kuwa kikundi kile kinachoshinikiza kung’olewa kwa Mkuyu ni sawa na kikundi kilichosababisha machafuko mlimani miaka ya nyuma..
Wazee hao wameapa kuendeleza shughuli za kung’oa mti huo licha ya pingamizi kutoka kwa mbunge Kapondi, wakisema ikiwalizimu watatumia mbinu nyingine .
Mti huo kufikia Jumatano ulikuwa umelindwa na Maafisa wa Polisi.
Written by, Wanji Sostine |