Pana haja ya vyama vya kisiasa katika eneo la Ukambani kushirikiana kwa pamoja, ili Jamii hiyo iwe na ushawishi mkubwa katika masuala ya uongozi wa kitaifa
Kiongozi wa Chama cha Liberal Party Augustus Muli akizungumza katika hafla kusajili wanachama, amesikitika kuwa kuna vyama zaidi ya kumi na vitatu katika eneo hilo ambavyo vinatofautiana kisera. Anasema hali hiyo inadhoofisha pakubwa umoja wa Jamii hiyo.


Aidha Muli amehimiza ushirikiano wa viongozi wa vyama hivyo na kuweka tofauti zao kando kwa ajili ya ustawi wa jamii ya Wakamba, ambayo kwa muda mrefu imekuwa katika upinzani bila mafanikio makubwa ya kimaendeleo.
“Kuna vyama zaidi ya kumi na kumi tatu hapa ukambani,tukishikana pamoja tutateua kiongozi mmoja atakaye gommbea kiti cha urais Mwaka elfu saba.Kama tutaendelea kukaa na tofauti zetu,itakuwa vigumu kwa Jamii hii kuwa na mwelekeo wa kisiasa,” Muli alionya.
Haja yanajiri wakati ambapo viongozi wa eneo la Ukambani wanamshiniza kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kuwania urais katika uchanguzi ujao wa mwaka wa 2027, bila kutegemea uungwaji mkono na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga
Kwa muda mrefu, Kalonzo amekuwa akimuunga mkono Raila kuwania kiti cha urais, kisha kumuacha nje na kuingia serikalini.
Writtem by, Raphael Mulatya