Naibu Gavana wa Machakos Francis Mwangangi amesema haitakuwa rahisi kwa Rais William Ruto kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 akiwataka wafuasi wake ”kuacha ndoto za mchana.”
Mwangangi, ambaye amewakosoa wafuasi wa rais hasa wa eneo la Bonde la Ufa kuwa Rais atashinda tena kwa muhula mwingine hata kama kura hazitakuwa za kutosha.
Alisema kuwa hii ni kauli za kichochezi na hatari zinazoweza kuingiza nchi katika mgogoro.
“Given how bitter Kenyans are united against Ruto there will be no leeway for him to return to office come 2027, hence such characters should stop day dreaming” he said adding that if a super power President Ronald Trump was one time rejected who is Ruto to must capture Presidency when Kenyans have said no.” alisema Mwangangi
Alisema umoja wa sasa miongoni mwa Wakenya sio wa upinzani pekee bali ni wa Wakenya wote wanaotaka mabadiliko ya uongozi 2027.
Aliongeza ” In this case people from Rift valley should swallow the bitterness and wait for majority of Kenyans decision” he added.”
Naibu Gavana alionya pia utawala wa Kenya Kwanza dhidi ya kuingilia uhuru na haki za uhuru wa vyombo vya habari nchini kama inavyoelekezwa na katiba.
Alisema, “Terrorizing Media houses because of highlighting the ills the government is doing to citizens is total violation of the constitution.”
Alivitaka vyombo vya habari vinavyolengwa kutokata tamaa, bali kuendelea kupigania haki za Wakenya.
Alisema haya wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu kwenye Kanisa Kuu la Katoliki la Machakos.