Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kupatikana na gramu 290 za dawa ya kulevya aina ya ‘cocaine’ katika eneo la Moyale, Kaunti ya Marsabit.

Kukamatwa kwa mwanamke huyo kufuatia msako maalum uliotekelezwa na kikosi cha usalama, kikilenga njia za usafirishaji wa mihadarati kati ya eneo la Kaskazini mwa Kenya na Nairobi.

Kwa mujibu wa polisi, dawa hizo ni za thamani ya takriban shilingi milioni moja.

Mshukiwa alikamatwa katika kizuizi cha barabarani kwenye barabara ya Moyale-Nairobi, wakati maafisa walipoisimamisha basi moja lililokuwa likielekea Nairobi kwa ukaguzi wa kawaida.

Kulingana na Idara ya Upelelezi DCI, tabia ya mshukiwa huyo iliwashangaza maafisa, hali iliyowalazimu maafisa wa kike kumtenga kwa uchunguzi wa kina wa mwili wake.

Katika upekuzi huo, maafisa walibaini kuwa gramu 294 za ‘cocaine’ zilikuwa zimefichwa kwa ujanja mkubwa katika sehemu zake za siri, katika oparesheni hiyo ya Ijumaa.

Taarifa ya DCI ilisema, ”Exhibiting behaviour signaling to “the guilty ones are always afraid”, female law enforcers isolated the 28-year-old for a thorough search, thereby confirming their suspicio.”

Mwanamke huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Moyale ambako anazuiliwa huku maafisa wa DCI wakijiandaa kumfungulia mashtaka.