Maafisa wa Polisi katika eneo la Kisumu Mashariki wanamtafuta mwanaume anayesemekana kumjeruhi vibaya mpenzi wake wa zamani kwa kumkatakata.
Kulingana na taarifa ya Polisi Mshukiwa Sebi Obonyo, alimvamia mpenzi wa zamani mwenye umri wa miaka ishirini na minne kwa sababu alimwacha na kuanza uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.
Obonyo anasemekana kumvamia mwanamke huyonyumbani kwa mpenzi wake wa sasa katika kijiji cha Nyakbong’ eneo la Kamjulu Ijumaa jioni kisha kimkata sikio na kumdunga kifuani.
Polisi wanaendeleza msako mkali dhidi ya mshukiwa anayesekemana kuwa mafichoni. Mwanamke aliyejeruhiwa anaendelea kutibiwa.