Hafla ya kuwatafuta wanamitindo inayoandaliwa na shirika la Mary Biketi ilikumbwa na ghasia baada ya kundi la vijana kuvamia ukumbi wa hafla hiyo na kuwatawanya waliokuwa wakishiriki.
Biketi, ambaye ni mpenzi wa Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya, alikuwa akiongoza hafla hiyo Ijumaa alasiri mjini Kitale kwa lengo la kupata wanamitindo watakaowakilisha shirika lake.
Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla baada ya gari lisilotarajiwa kuwasili. Muda mfupi baadaye, vijana waliokuwa na visu na panga walivamia hafla hiyo.
Biketi alilaani vikali tukio hilo, “The first time I was here, I did something for the elderly, and this time around, I thought I would do something for the youth, then this happened. We were going on with our program when the goons came in…they started beating us, robbing us, and even broke vehicles,” alisema
Alisisitiza kuwa yeye si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa bali nia yake ni kusaidia jamii.
Alisema, “We are not in any political party; we just want to help each other. We are empowering women, youths, and the vulnerable.”
Waandalizi wengine waliokuwa pamoja naye pia walilaani tukio hilo, wakitoa wito kwa vijana kujiepusha kutumiwa na wanasiasa wenye misimamo ya kugawa watu.
Biketi si jina geni katika nchini, kwani alijulikana zaidi kufuatia uhusiano wake na aliyekuwa Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya. Katika mahojiano ya awali, Oparanya alithibitisha uhusiano huo na kusema wake zake wawili wanafahamu na hawana pingamizi.

Biketi aliondolewa salama kutoka eneo la tukio baada ya usalama wake kuhakikishwa.